Saturday 21 February 2015

NYINGE NAZARENO NJIA PANDA KUGOMBEA DODOMA MJINI AU KALENGA




 
 
Nazareno Nyinge: Anasema
"Wakati nafanya tathmini ndogo ya kusimama kupigania jimbo la dodoma mjini naangalia kwa jicho la mwewe jimboni kwangu nilikozaliwa KALENGA ambapo fadhila zimetumika kurithisha madaraka pasipo kujali huruma ya wananchi wanaotaka mabadiliko napata shida sana na cjui nisimame wapi kote hali ngumu

1. wanawake wanapata shida mahospitalini

2. miundombinu kwao ni hadithi husikia kwenye taarifa ya habari tena kupitia radio ya m/kiti wa mtaa

3. huduma za jamii nashukuru kwa kuwa mungu aliweka vyanzo vya maji hivyo wanakunywa maji meupe yasiyo salama

4. kufanya mabadiliko wanatishiwa kutatokea vita

5. kofia na khanga imekuwa ndiyo hongo kwao

6. napata uchungu kuona wanafunzi wanakaa chini mpaka miaka zaidi ya 50 baada ya kuwa huru

7.kenya wanafanya jitihada angalau kila mwanafunzi awe na computer yake wakati tanzania tunasema angalau kila mwanafunzi awe na dawati

nathubutu bila kuwa na maslahi yeyote kwamba sintoacha hata chembe ya sekunde ya muda kupotea nitapigana mpaka mabadiliko ya kweli na ukombozi wa kweli unapatikana

vijana tubadilishe fikra zetu kwa kutokujikitaa sana kushabikia vyama tuweke watu wanaoweza kuleta mapinduzi ya kweli

viwanda kurudisha

rasili mali kupewa nafasi kutumika na wananchi tabaka zote kwa usawa

wananchi kujivunia kile kilichochao daima....young generation forever...

No comments:

Post a Comment