Friday 6 March 2015

MAAMUZI MAGUMU YA MWAL. NYRERE ENZI ZA UHAI WAKE

 

 

MAAMUZI MAGUMU YA MWALIMU NYERERE

1. Idd Amini - Alipoivamia Tz.... Mwalimu
alitamka tutampiga nduli!.. Na kweli Idd Amini
alipigwa hadi akaikimbia Uganda....
2. Kolimba - Alipotamka CCM imepoteza Dira na
Mwelekeo... Mwalimu alimwita Dodoma
akamuuliza nani kakutuma useme hivyo?!.. Ndio
ukawa mwisho wa Kolimba!..
3. Samweli Sitta - Alipokuwa kiongozi wa serikali
ya wanafunzi UDSM aliongoza mgomo wa
wanafunzi wenzake kudai siagi na maziwa!...
Mwalimu aliibuka pale chuoni akamuuliza
Samweli Samweli kwenu mnakunywa maziwa
kweli?!.. Akamwambia lala chini, akamcharaza
bakora na mgomo ukaishia hapo hapo!...
4. Abdul Jumbe! - Alipotaka serikali tatu!..
Nyerere alimuuliza moja kujumlisha moja ni
ngapi?!.. Jumbe akajibu ni mbili!.. Nyerere
akamwambia kama ni mbili mbona unataka
serikali tatu?!.. Huo ndio ukawa mwisho wa
Abdul Jumbe kuwa Rais wa Zanzibar!..
5. John Samwel Malecela - Ni baada ya taarifa
kuzagaa kuwa amebadili dini na jina ili apate
kuungwa mkono na nchi za kiislamu kugombea
Urais mwaka 1995!.. Nyerere alimwambia wee
John wewe umeenda Arabuni mara moja
umebadilisha jina sasa unaitwa Jumanne!.
Ukienda mara ya pili si utabadilisha kabila?!...
Huo ukawa mwisho wa ndoto zake kuwa Rais wa
Tz !...
6. Edward Lowassa - Alipokodi ndege binafsi
ikampeleka hadi dodoma kwenye vikao vya
mchujo wa wagombea Urais kupitia CCM mwaka
1995 alimpa lift JK!.. Nyerere alimuuliza
mmekuja na Ndege dodoma pesa mmetoa
wapi?!.. Jina la Lowassa likakatwa kabla ya vikao
vya mchujo!.. . Natamani Nyerere angekuwepo
sasa na mwaka 2015!

Monday 23 February 2015

ANGALIA KILICHOTOKEA LEO NJE YA BUNGE LA UKRAINE WAZICHAPA NJE NJE







Ona kilichotokea katika Nje ya bunge la UKRAINE ,,, je ni demokrasia imezidi au haipo kabisa


JESHI LA POLISI LPATA WASIWASI JUU YA VIKUNDI VYA USALAMA VYAMA VYA SIASA


 

 

  kikundi cha usalama cha CHADEMA



JESHI la Polisi nchini limetangaza kuanza uchunguzi dhidi ya vikundi vyote vya ulinzi na usalama vinavyoanzishwa na vyama vya siasa nchini.
Pamoja na hili limesema kuwa litachunguza kwa kina mafunzo yanayotolewa na vyama hivyo kama yanahusiana na shughuli za kijeshi au laa.
Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi imekuja siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuzindua kikundi cha Ulinzi na Usalama (Red Brigade) katika mikoa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza na mwandishai  wa  habari  jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu alisema kuwa, sheria za nchi zimeweka wazi namna ya kuwapo kwa vikundi vya ulinzi na usalama na si kila mtu anaweza kuanzisha kikundi chake.
Alisema licha ya baadhi ya vikundi kutambulika lakini vingi hufanya kazi kwa utaratibu na kwa mujibu wa sheria za nchi.
IGP Mangu alisema hatua ya kila chama kuanzisha kikundi chake inaweza kusababisha vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Alisema kutokana na hali hiyo ni lazima Jeshi la Polisi liwe makini wakati wote kwa kuhakikisha wanafuatilia mwenendo vya vikundi hivyo na madhumuni ya kuanzishwa kwake.
“Tutachunguza vikundi hivyo ili tuweze kubaini mafunzo wanayopewa kama yanafanana na mafunzo ya vikosi vya ulinzi na usalama vinavyofanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi. Katiba ya nchi inavitambua vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
“Kuanzishwa kwa vikundi vidogodogo ndani ya vyama vya siasa ambavyo vinafanya kazi ya ulinzi na usalama vinaweza kuhatarisha amani ya nchi, lazima tuchunguze ili tuweze kubaini mafunzo wanayopewa kama yanafanana na vikosi vya ulinzi na usalama au la, hapo tutajua ukweli zaidi,”alisema IGP Mangu.
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi alisema katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani jeshi la polisi limejipanga kudhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani ambavyo vinaweza kuhatarisha hali ya usalama wa nchi na watu wake.
Alisema kutokana na hali hiyo, watahakikisha kuwa vikundi vinavyoanzishwa havifanyi kazi ya ulinzi na usalama kwa sababu siyo jukumu lao.
“Lazima tuwe makini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuhakikisha kuwa vikundi hivi vinavyoanzishwa haviwezi kuhatarisha amani ya nchi,” alisema.
Msajili aonya
Akizungumzia suala hilo, Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alisema kuwa, sheria ya vyama vya siasa hairuhusu kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi na usalama, ila wanasiasa wamekuwa wakitafsiri tofauti.
Alisema kuna mambo mengi yanayofanywa na wanasiasa ambayo wanavunja sheria za nchi, lakini wanashindwa kujirekebisha na kujiona wako sahihi.
Alisema kutokana na hali hiyo, suala hilo ni nyeti sana, hivyo wanatakiwa kuelimishwa kwa kina ili waweze kujua majukumu yao ya chama na shughuli nyingine ambazo haziwahusu.
“Unajua hili suala ni nyeti sana, huwezi kulizungumzia ki uwepesi wepesi, kwa sababu lina upana wake, lakini wanasiasa wanalichukulia kikawaida bila ya kuangalia athari zake baadaye,”alisema Jaji Mutungi.
Aliongeza kuna matatizo mengi ya upotoshaji wa kisheria ndani ya vyama vya siasa, jambo ambalo linaweza kusababisha migongano ya wenyewe kwa wenyewe.
Alisema kutokana na unyeti wa suala hilo hawezi kulizungumzia kwa ufupi kwa sababu kuna masuala ya kisheria ambayo yanapaswa kufafanuliwa kwa kina zaidi ili jamii iweze kutambua ukweli kuhusu suala hilo.
“Lazima ifike kipindi vyama vya siasa vifuate matakwa ya sheria ya nchi kwa sababu ndiyo sheria mama inayoongoza nchi, bila ya kufanya hivyo tutakuwa tunavunja sheria kila siku,”alisema Jaji Mutungi.
Kwa muda mrefu vyama vya siasa hasa vya CCM, Chadema na CUF vimekuwa vitoa mafunzo kwa vijana wake kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi.
Mbali ya Chadema inayomiliki Red Brigade, CCM inamiliki kikundi cha Green Guard, huku cha CUF ikimiliki kikundi cha Blue Guard.

ANGALIA WANAJESHI WA JKT WALIOKOSA AJIRA WALIVYOENDA KUMJULIA HALI MUHIMBILI BAADA YA KUTEKWA



Mwenyekiti wa JKT, George Mgoba akiwa wodini.
Askari wakiimarisha usalama eneo la 
 Hospitali ya Muhimbili.
Baadhi ya askari wa JKT wakiwasili Muhimbili.
Baadhi ya wanajeshi wa JKT wakiingia hospitalini.
VIJANA mbalimbali ambao walipata mafunzo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), leo wamekutana katika eneo la Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, kisha kuelekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kumjulia hali mwenyekiti wao George Mgoba ambaye alitekwa na watu wasiojulikana.
GPL ilifanikiwa kufika eneo la Msimbazi Center walipokusanyika askari hao na baadaye kuelekea Hospitali ya Muhimbili. Hata hivyo, wanahabari walishindwa kuzungumza na mwenyekiti huyo kwa sababu za kiusalama.

VITA VYA URAIS CCM NJE NJE ... VIJANA KWA WAZEE WAPIGANA VIJEMBE









Sadifa Juma Hamisi 

Na Mussa Juma, Mwananchi
Arusha. Wakati joto la urais likizidi kupanda ndani ya CCM kutokana na hofu ya baadhi ya majina mazito ya wagombea wa nafasi hiyo kukatwa kwa mizengwe, vita vya wagombea sasa ni dhahiri baada ya mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kusema hakuna mtu atakayekatwa bila ya sababu za msingi.
Mjumbe huyo, Sadifa Juma Hamisi, ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), pia alisema umoja huo haujafikia uamuzi wala kumtuma mtu kumdhibiti mwanachama anayetajwa kuwania urais.
Katika siku za karibuni kumekuwapo mjadala mkubwa ndani ya CCM juu ya mtu atakayepitishwa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho, na ilizidi baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa mwanachama ambaye atateuliwa na CCM kugombea urais hayumo miongoni mwa waliojitokeza na kuwataka wanachama kuwashawishi watu wenye sifa wajitokeze.
Siku chache baadaye, Dk Raphael Chegeni aliliambia gazeti la Mwananchi kuwa ametumwa na wanachama wa CCM wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda kumshawishi Lowassa kujitokeza kuwania urais kuitikia wito wa Rais Kikwete wa kuwataka wanachama kuwashawishi watu wenye sifa kujitokeza.
Hadi sasa, wanachama waliojitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea urais ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, January Makamba (Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia), Hamisi Kigwangala, na Lazaro Nyalandu ambaye ni waziri wa Maliasili na Utalii.
Lakini pia wako wanaotajwa kuwania urais lakini hawajatangaza ambao ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sita, William Ngeleja, Emmanuel Nchimbi, Mwigulu Nchemba, Stephen Wasira, Bernard Membe na Edward Lowassa ambaye ameibua mjadala kati ya kambi yake na zinazompinga.
Mapema wiki iliyopita, katibu wa uhamasishaji na chipukizi wa UVCCM, Paul Makonda alikaririwa akisema kuwa vitendo vyake vya kumshambulia Lowassa vinatokana na kutumwa na umoja huo kumdhibiti, jambo ambalo limezidisha mjadala kuhusu mteule wa chama hicho.
Kutokana na hofu hiyo, viongozi wa UVCCM na CCM mkoani Arusha wametuma ujumbe wa maneno kwa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa za chama hicho wakitaka wanachama wasifanyiwe kile wanachokiita kuchafuana na vitisho vya baadhi ya wagombea kukatwa kimizengwe.
Ujumbe huo ulitumwa juzi na mwenyekiti wa CCM wa mkoa, Onesmo ole Nangole na mwenyekiti wa UVCCM, Robinson Meitinyiku ambao walitaka Sadifa Juma Hamis kueleza msimamo wa mkoa kwa vyombo hivyo viwili vya maamuzi, na mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM aliwahakikishia kuwa hakuna mgombea atakayekatwa kwa “sababu za kijinga”.
Akijibu ujumbe wa viongozi hao, Sadifa aliyekuwa jijini hapa kumsimika kamanda wa vijana wa wilaya ya Arumeru, Mathias Manga, aliwaondolea hofu katika hafla hiyo akisema hakuna mgombea wa urais wa CCM ambaye atakatwa bila sababu za msingi, lakini akawataka vijana kusubiri zamu yao hadi 2025.
Kauli ya Sadifa


“Niwaombeni mwenyekiti wa mkoa na mwenyekiti wa UVCCM, msiogope. Hakuna mtu atakayekatwa kijinga ndani ya Kamati Kuu au Halmashauri Kuu. Kikubwa tufuate maadili. Mimi mchapakazi ndiye nitamtetea,” alisema bila kutaja mgombea anayekusudiwa.Alisema ni lazima kiongozi bora awe na mikakati na dira na upeo wa kuwa na mikakati bora ya kutekeleza ahadi zake kwani hatuwezi kuwa na kiongozi ambaye hana dira wala mikakati.
“Tunataka kiongozi mwenye kujiamini, awe ana vision (dira) na mission (mikakati), msikivu... hatuwezi kuchagua rais ambaye hana sifa hizi,” alisema.
Akizungumzia maombi ya Nangole kuhusu tabia ya kuwachafua baadhi ya wagombea na kuwatisha, Sadifa alisema hakuna kiongozi aliyetumwa na CCM na UVCCM kutukana mtu wala kumtisha.
“Mzee wangu, watu wengi wanajua wanamtaka nani, ukiona mtu anapanda kwenye majukwaa anamchafua mwenzake, ujue huyo ana mapungufu ya malezi, hakuna haja ya kumjibu kwani utaonekana na pia wewe una mapungufu,” alisema.
Akionekana kujibu kauli ya Makonda, Sadifa alisema UVCCM haijatuma mtu amtukane mwingine. Alisema akiwa mjumbe wa Kamati Kuu, hawajawahi kumtuma kiongozi yoyote kumtukana mwanachama mwingine wa CCM.
Alipoulizwa kuhusu hofu hiyo, kwa kifupi katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: “Mimi siwezi kuwa msemaji wa Umoja wa Vijana, nikisema niwajibu nitakuwa nimepotoka.”
Mapema wiki iliyopita, Makonda alikaririwa akisema kuwa amekuwa akimshambulia Lowassa, ambaye anatajwa kuwania urais kupitia CCM, kwa sababu ametumwa na umoja huo.
Makonda amekuwa akikaririwa mara kwa mara akisema kuwa Lowassa hafai kuwa mteule wa CCM wa kuwania urais na mikanda ya kauli zake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, jambo lililofanya uteuzi wake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni uhojiwe na watu wengi na hivyo kujikuta akilazimika kusema ametumwa na umoja wake kumdhibiti waziri mkuu huyo wa zamani.
Katika mazungumzo yake juzi, Sadifa hakutaka kutaja jina la mgombea atakayemtetea wala mtu anayemshambulia, badala yake alisema muda ukifika, kila kitu kitajulikana kwa kuwa watu wanamjua mgombea wanayemtaka.
“Mwenyekiti, dawa ya mjinga ni kukaa kimya, watu wanamjua mtu ambaye wanamtaka. Rais Jakaya Kikwete ni mtu ambaye hatabiriki, hana ushemeji... nyie subirini tu wakati ukifika,” alisema.
Vijana na urais
Akizungumzia vijana ambao wanautaka urais, Sadifa aliwataka kusubiri zamu yao hadi 2025 ili wazee waliopo wamalize muda wao.

Alisema utakapofika mwaka 2025 vijana watakuwa katika nafasi nzuri sana ya kushika uongozi na hawatakubali kuona viongozi wazee wakitaka kupewa nafasi.
“Wazee tutawaomba radhi mwaka wenu ni 2015 hadi 25, mkimaliza hapo, miaka yenu imekwisha, msije tena,” alisema.
Kauli ya Nangole
Awali, Nangole, ambaye aliwahi kusema kuwa Lowassa ni kiongozi msikivu na makini na ambaye ni tegemeo la Watanzania katika kuwaunganisha kuwa kitu kimoja, aliomba Kamati Kuu ipelekewe ujumbe kuwa CCM mkoani Arusha hairidhishwi na matendo ya baadhi ya viongozi kuwatukana na kuwatisha wengine.
Nangole alirejea kauli aliyowahi kuitoa kuwa CCM ni ya wanachama wote na ndani yake hakuna sisimizi au tembo wa kumtisha mwingine ili mradi anafuata taratibu za chama hicho.
Alisema imeibuka tabia ya baadhi ya viongozi wa CCM, kuwatisha wengine na kuwatukana kana kwamba wao ndio wana hatimiliki ya CCM.
Naye mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha, Robinson Meitinyiku alisema kuna kiongozi mmoja ametoa kauli kuwa mgombea mmoja hata kama akisafishwa na madodoki hawezi kuwa msafi.
Badala yake alisema kiongozi aliyetoa maneno hayo ndiye hawezi kusafishika hata kwa gunzi kwani kuna taarifa aliwahi kusaliti na kujiunga na chama kingine.

MAGAZETI YA LEO JUMATATUTU 23/2/2015


 DSC09824



































http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/02/DSC09827.jpg


 .



.


 .

 .

 .


 .

 .

 .


 .


 .

 .

.

 .

 .

 .

 ..

 .



 .


 .

 .

 .

 .

.