Wednesday 18 February 2015

ALICHOKISEMA KADA WA CHADEMA KUHUSU UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA

 
Nimepitia orodha ya wakuu wa wilaya sijaona jipya hususani kwenye kanda yangu ya DSM na mkoa wa Kinondoni, nimemuona mtu anayeitwa @paul makonda eti naye ni mkuu wa wilaya.
Namkaribisha sana kwenye mkoa wa kinondoni wenye majimbo matatu, mawili ya kiwa ni Chadema na moja ni ccm kwa bahati mbaya sana.
Hapa kama mnavyojua vyeo hivyo mmepewa kisiasa mtakavyo kuja ndivyo tutakavyo wapokea, lazima mjue mpo kwenye himaya ya Chadema na sivinginevyo kama mlivyoaminishwa.
Tutafanya siasa za level nyingine mtakayo ichagua.
Uko kwenye himaya ya chadema uropokaji wako uishie huko, hapa mtatii mamlaka ya Chadema, kutoonea watu, kutisha watu, kubambikia watu kesi za uongo, vile vile Kinondoni tulikuwa tumesahau uwizi wa simu zetu za mkononi umepungua kabisa, tunategemea kuwa hili la uwezi wa simu halitajitokeza huku uraiani kwani huku huwa tunaonaga kwenye vyombo vya habari kuwa Wananchi wenye hasira kali wamechoma kibaka aliyepora simu. Hakunaga mwongozo wanamna ya kushughulika na kibaka wa simu.
Wabunge wangu na madiwani wetu wamejitahidi sana kupigania viwanja vya wazi virudi na vimerudi hatutegemei kinondoni kuwa kichaka cha wanyang'anyi wa Ardhi, huwa tukidhulumiwa hatusiti kupiga peoples power mpaka nyumbani.
HII NDIYO KINONDONI HUWA HATUSUBIRI KUAMBIWA NAMNA YA KUDAI HAKI YETU
HENRY KILEWO
KATIBU KINONDONI/DSM
CHADEMA..

1 comment: