Friday 20 February 2015

KAULI NZITO YA KADA WA CHADEMA JUU YA MAUUWAJI YA ALBINO



Remija Wa Yesu
Nimesikitishwa sana na mauaji ya mtoto Yohana Bahati!! Mauaji ya kinyama kabisa, ninalaani mauaji haya.
Ninachojiuliza kama serikali inatumia pesa nyingi kujenga mahospitali na kuajiri madaktari, na inasema haiamini katika uchawi, sasa hawa waganga wa kienyeji na wachawi wanatoka wapi? Kwanini wanasajiriwa? Kwanini wapo kwa tiba zipi? Mbona haya mahospitali hawajawahi kutoa rufaa wagonjwa waende kutibiwa kwa waganga wa kienyeji?
Utasikia watasema tuwalinde albino, tuwapeleke kwenye mashule fulani, tusiwaache peke yao, kwanini hawa wachawi wasizuiliwe kufanya kazi zao? Watu wajiishie kwa rahaaa.
Ninachoshangaa na kujiuliza zaidi watanzania wote isipokuwa wachache sana: niliwahi kuambiwa, nilipokuwa mdogo Kingunge tu ndio haamini katika dini hizi, ila sijathibitisha mpaka leo, na katika kukua kwangu mpaka leo sijakutana na MTU mpagani, ila wote sisi ni wakristo na waislamu tena waumini wazuri wa kuhudhuria kwenye nyumba za ibada, inakuwaje hawa waganga wapo na wanapata wateja? Ni Mungu yupi tunayemwabudu? Au ndio michanganyo, mungu baali kidogo na Mungu muumba Mbingu na Nchi kidogo.
Ningekuwa rais ningefutulia mbali waganga wote.
RIP Yohana Bahati kilio cha damu yako kitafika Mbinguni!!!!!

No comments:

Post a Comment