Nazareno Nyinge: Anasema
"Wakati
nafanya tathmini ndogo ya kusimama kupigania jimbo la dodoma mjini
naangalia kwa jicho la mwewe jimboni kwangu nilikozaliwa KALENGA ambapo
fadhila zimetumika kurithisha madaraka pasipo kujali huruma ya wananchi
wanaotaka mabadiliko napata shida sana na cjui nisimame wapi kote hali
ngumu
1. wanawake wanapata shida mahospitalini
2. miundombinu kwao ni hadithi husikia kwenye taarifa ya habari tena kupitia radio ya m/kiti wa mtaa
3. huduma za jamii nashukuru kwa kuwa mungu aliweka vyanzo vya maji hivyo wanakunywa maji meupe yasiyo salama
4. kufanya mabadiliko wanatishiwa kutatokea vita
5. kofia na khanga imekuwa ndiyo hongo kwao
6. napata uchungu kuona wanafunzi wanakaa chini mpaka miaka zaidi ya 50 baada ya kuwa huru
7.kenya wanafanya jitihada angalau kila mwanafunzi awe na computer yake
wakati tanzania tunasema angalau kila mwanafunzi awe na dawati
nathubutu bila kuwa na maslahi yeyote kwamba sintoacha hata chembe ya
sekunde ya muda kupotea nitapigana mpaka mabadiliko ya kweli na ukombozi
wa kweli unapatikana
vijana tubadilishe fikra zetu kwa kutokujikitaa sana kushabikia vyama tuweke watu wanaoweza kuleta mapinduzi ya kweli
viwanda kurudisha
rasili mali kupewa nafasi kutumika na wananchi tabaka zote kwa usawa
wananchi kujivunia kile kilichochao daima....young generation forever...
No comments:
Post a Comment