Wednesday 18 February 2015

WB: Tanzania imetoka kundi la nchi masikini zaidi

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/2aa0c429d490d6a5f964b4957d8eb79e_XL.jpg
Ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia (WB) inaonesha kuwa, nchi ya Tanzania haiko tena katika kundi la nchi 10 masikini zaidi duniani. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, ripoti hiyo imezingatia pato la taifa, ambalo kimsingi huwa ni jumla ya thamani ya bidhaa zilizozalishwa kwa kipindi fulani, mara nyingi kwa mwaka, kikigawanywa kwa idadi ya watu ndani ya nchi husika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi 10 maskini zaidi duniani ni Malawi, ambayo pato la kila mwananchi wa taifa hilo kwa mwaka, ni dola za Kimarekani 226.50. Malawi inafuatiwa na Burundi, Dola 267.10, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Dola 333.20, Niger, Dola 415.40, Liberia, Dola 454. 30 na Madagascar, Dola 463. Aidha mataifa mengine na pato la kila mwananchi, ni ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Dola 484.20, Gambia, Dola 488.60, Ethiopia, Dola 505, na nchi ya 10 kwa umaskini ni Guinea, ambako pato la mwananchi ni Dola 523.10. Akizungumzia sababu zilizochangia Tanzania kuondoka kwenye kundi hilo la nchi 10 maskini zaidi duniani, Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Haji Semboja amesema kuwa, hilo linaonyesha kuwa Tanzania imeweza kujenga uwezo wa kuzimiliki, kuzisimamia, na kuziendesha rasilimali nyingi ilizojaaliwa, ili kuboresha ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment