Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa
wanapanga kuchapisha majina ya takriban watu 200 wanaotuhumiwa kuendesha
uhalifu wa kivita nchini Syria.
Tume huru ya uchunguzi ya umoja wa mataifa inasema kuwa kumekuwa na ongezeko la uhalifu nchini humno.
Majina
yanayojumuisha wakuu wa kijeshi , wasimamizi wa magereza na makamanda
wa makundi yasiyokuwa ya serikali yaliyo na silaha tayari yamewasilishwa
kwa tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa.
Serikali ya Syria hatahivyo imekataa kutoa ushirikiano kwa tume hiyo.
Umoja
wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 220,000 wameuawa nchini Syria na
mamilioni ya wengine wamehama makwao wakati wa mazozo wa miaka minne .
No comments:
Post a Comment