KUFUATIA mapigano makali katika mji wa Mashariki ya
Ukraine,baraza la usalama la Umoja wa mataifa limehimiza makubaliano ya
kuweka chini silaha yaheshimiwe haraka.
Muswada wa azimio uliowasilishwa na Urusi umezitaka pande zote
zinazohasimiana zitekeleze makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita mjini
Minsk.
Tayari Wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wameliangalia azimio hilo
kuwa ni ushindi kwa sababu kwa mara ya kwanza mataifa yote 15 Wachama wa
Baraza la Usalama wameyatambua matokeo ya mkutano wa Kilele wa Minsk
No comments:
Post a Comment