WAZIRI wa Nishati na Madini,mheshimiwa 
GEORGE SIMBACHAWENE amefanya ziara mkoani Lindi na Mtwara mwanzoni mwa 
wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Wizara yake ambapo 
ameahidi huduma za umeme na Maji kwa wananchi mbalimbali.
Akiwa Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya 
Maendeleo ya Ujenzi wa Mtambo wa kuchakata gesi, Waziri SIMBACHAWENE 
amemwagiza Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi KAPUULYA 
MUSOMBA kutoa huduma ya Maji Safi kwa Wananchi wanaozunguka maeneo hayo.




 
 
No comments:
Post a Comment