Remija Wa Yesu
Nimesikitishwa sana na mauaji ya mtoto Yohana Bahati!! Mauaji ya kinyama kabisa, ninalaani mauaji haya.
 Ninachojiuliza kama serikali inatumia pesa nyingi kujenga mahospitali 
na kuajiri madaktari, na inasema haiamini katika uchawi, sasa hawa 
waganga wa kienyeji na wachawi wanatoka wapi? Kwanini wanasajiriwa? 
Kwanini wapo kwa tiba zipi? Mbona haya mahospitali hawajawahi kutoa 
rufaa wagonjwa waende kutibiwa kwa waganga wa kienyeji? 
Utasikia watasema tuwalinde albino, tuwapeleke kwenye mashule fulani, tusiwaache peke yao, kwanini hawa wachawi wasizuiliwe kufanya kazi zao? Watu wajiishie kwa rahaaa.
Utasikia watasema tuwalinde albino, tuwapeleke kwenye mashule fulani, tusiwaache peke yao, kwanini hawa wachawi wasizuiliwe kufanya kazi zao? Watu wajiishie kwa rahaaa.
 Ninachoshangaa na kujiuliza zaidi watanzania wote isipokuwa wachache 
sana: niliwahi kuambiwa, nilipokuwa mdogo Kingunge tu ndio haamini 
katika dini hizi, ila sijathibitisha mpaka leo, na katika kukua kwangu 
mpaka leo sijakutana na MTU mpagani,  ila wote sisi ni wakristo na 
waislamu tena waumini wazuri wa kuhudhuria kwenye nyumba za ibada, 
inakuwaje hawa waganga wapo na wanapata wateja? Ni Mungu yupi 
tunayemwabudu? Au ndio michanganyo, mungu baali kidogo na Mungu muumba 
Mbingu na Nchi kidogo.
Ningekuwa rais ningefutulia mbali waganga wote.
RIP Yohana Bahati kilio cha damu yako kitafika Mbinguni!!!!!
Ningekuwa rais ningefutulia mbali waganga wote.
RIP Yohana Bahati kilio cha damu yako kitafika Mbinguni!!!!!

No comments:
Post a Comment