Mwili wa mtoto Yohana Bahati
aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja ambaye ni mlemavu wa ngozi maarufu kama
Albino, alitekwa siku ya Jumapili February 15, 2015 amepatikana ameuawa
katika eneo la Shilabela Mapinduzi kilomita kadhaa kutoka nyumbani kwao
kijiji cha Ilelema .Polisi wanaeleza kuwa waliukuta mwili huo katika
msitu wa hifadhi wa Biharamulo leo majira ya alfajiri akiwa amekatwa
mikono na miguu yake.
Wakati mwili wa mtoto Yohana ukipatikana
,mama wa mtoto huyo bi , Ester Jonas mwenye umri wa miaka 30 bado hali
ya afya yake ni tete na amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando ,
Mwanza . Madaktari walimfanyia upasuaji mwanamke huyo aliyekuwa amekatwa
kwa panga usoni mwake na sehemu zingine za mwili majeraha ambayo
aliyapata wakati alipokuwa akijaribu kumuokoa mwanawe, Yohana kutoka
mikononi mwa wauaji .
Dada zake Yohana Tabu bahati mwenye umri wa
miaka mitatu bado yuko mikononi mwa uangalizi wa askari polisi. Dada yao
mkubwa ambaye pia ni Albino Shida Bahati mwenye umri wa miaka kumi na
miwili amehamishwa kijijini hapo tangu tukio hilo litokee, na anatunzwa
na jamaa zake katika kijiji jirani.
Mpaka sasa watu wengine wawili
zaidi wamekamatwa na polisi wakihusishwa na tukio hilo ingawa baba
mzazi wa mtoto huyo, bado anashikiliwa na polisi.
Mwezi uliopita
serikali ya Tanzania ilipiga marufuku waganga wa kienyeji pia kupiga
marufuku wapiga ramli wote ambao wanaelezwa kuchangia mauaji ya watu hao
wenye ulemavu wa ngozi.. waganga wa kienyeji wanaamini kwamba viungo
vya mwili wa Albino huleta bahati na utajiri kwa anaye vipata.katazo
hilo ni sehemu ya mkakati maalumu wa kupunguza kama sio kuondosha kabisa
mashambulizi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
No comments:
Post a Comment