Ona kilichotokea katika Nje ya bunge la UKRAINE ,,, je ni demokrasia imezidi au haipo kabisa
This site is about challenges facing world politically,socially,economically,environmentally and bring entrainment i.e soccer,Love matters,and news all over the world.....
Monday, 23 February 2015
ANGALIA KILICHOTOKEA LEO NJE YA BUNGE LA UKRAINE WAZICHAPA NJE NJE
Ona kilichotokea katika Nje ya bunge la UKRAINE ,,, je ni demokrasia imezidi au haipo kabisa
JESHI LA POLISI LPATA WASIWASI JUU YA VIKUNDI VYA USALAMA VYAMA VYA SIASA
kikundi cha usalama cha CHADEMA
JESHI
la Polisi nchini limetangaza kuanza uchunguzi dhidi ya vikundi vyote
vya ulinzi na usalama vinavyoanzishwa na vyama vya siasa nchini.
Pamoja na hili limesema kuwa litachunguza kwa kina mafunzo yanayotolewa na vyama hivyo kama yanahusiana na shughuli za kijeshi au laa.
Hatua hiyo ya Jeshi la Polisi imekuja siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuzindua kikundi cha Ulinzi na Usalama (Red Brigade) katika mikoa ya Kanda za Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza na mwandishai wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu alisema kuwa, sheria za nchi zimeweka wazi namna ya kuwapo kwa vikundi vya ulinzi na usalama na si kila mtu anaweza kuanzisha kikundi chake.
Alisema licha ya baadhi ya vikundi kutambulika lakini vingi hufanya kazi kwa utaratibu na kwa mujibu wa sheria za nchi.
IGP Mangu alisema hatua ya kila chama kuanzisha kikundi chake inaweza kusababisha vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Alisema kutokana na hali hiyo ni lazima Jeshi la Polisi liwe makini wakati wote kwa kuhakikisha wanafuatilia mwenendo vya vikundi hivyo na madhumuni ya kuanzishwa kwake.
“Tutachunguza vikundi hivyo ili tuweze kubaini mafunzo wanayopewa kama yanafanana na mafunzo ya vikosi vya ulinzi na usalama vinavyofanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi. Katiba ya nchi inavitambua vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo vinafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
“Kuanzishwa kwa vikundi vidogodogo ndani ya vyama vya siasa ambavyo vinafanya kazi ya ulinzi na usalama vinaweza kuhatarisha amani ya nchi, lazima tuchunguze ili tuweze kubaini mafunzo wanayopewa kama yanafanana na vikosi vya ulinzi na usalama au la, hapo tutajua ukweli zaidi,”alisema IGP Mangu.
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi alisema katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani jeshi la polisi limejipanga kudhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani ambavyo vinaweza kuhatarisha hali ya usalama wa nchi na watu wake.
Alisema kutokana na hali hiyo, watahakikisha kuwa vikundi vinavyoanzishwa havifanyi kazi ya ulinzi na usalama kwa sababu siyo jukumu lao.
“Lazima tuwe makini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa kuhakikisha kuwa vikundi hivi vinavyoanzishwa haviwezi kuhatarisha amani ya nchi,” alisema.
Msajili aonya
Akizungumzia suala hilo, Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alisema kuwa, sheria ya vyama vya siasa hairuhusu kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi na usalama, ila wanasiasa wamekuwa wakitafsiri tofauti.
Alisema kuna mambo mengi yanayofanywa na wanasiasa ambayo wanavunja sheria za nchi, lakini wanashindwa kujirekebisha na kujiona wako sahihi.
Alisema kutokana na hali hiyo, suala hilo ni nyeti sana, hivyo wanatakiwa kuelimishwa kwa kina ili waweze kujua majukumu yao ya chama na shughuli nyingine ambazo haziwahusu.
“Unajua hili suala ni nyeti sana, huwezi kulizungumzia ki uwepesi wepesi, kwa sababu lina upana wake, lakini wanasiasa wanalichukulia kikawaida bila ya kuangalia athari zake baadaye,”alisema Jaji Mutungi.
Aliongeza kuna matatizo mengi ya upotoshaji wa kisheria ndani ya vyama vya siasa, jambo ambalo linaweza kusababisha migongano ya wenyewe kwa wenyewe.
Alisema kutokana na unyeti wa suala hilo hawezi kulizungumzia kwa ufupi kwa sababu kuna masuala ya kisheria ambayo yanapaswa kufafanuliwa kwa kina zaidi ili jamii iweze kutambua ukweli kuhusu suala hilo.
“Lazima ifike kipindi vyama vya siasa vifuate matakwa ya sheria ya nchi kwa sababu ndiyo sheria mama inayoongoza nchi, bila ya kufanya hivyo tutakuwa tunavunja sheria kila siku,”alisema Jaji Mutungi.
Kwa muda mrefu vyama vya siasa hasa vya CCM, Chadema na CUF vimekuwa vitoa mafunzo kwa vijana wake kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi.
Mbali ya Chadema inayomiliki Red Brigade, CCM inamiliki kikundi cha Green Guard, huku cha CUF ikimiliki kikundi cha Blue Guard.

ANGALIA WANAJESHI WA JKT WALIOKOSA AJIRA WALIVYOENDA KUMJULIA HALI MUHIMBILI BAADA YA KUTEKWA
Mwenyekiti wa JKT, George Mgoba akiwa wodini.
Askari wakiimarisha usalama eneo la
Hospitali ya Muhimbili.
Baadhi ya askari wa JKT wakiwasili Muhimbili.
Baadhi ya wanajeshi wa JKT wakiingia hospitalini.
VIJANA mbalimbali
ambao walipata mafunzo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), leo
wamekutana katika eneo la Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, kisha
kuelekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kumjulia
hali mwenyekiti wao George Mgoba ambaye alitekwa na watu wasiojulikana.
GPL ilifanikiwa kufika eneo la Msimbazi Center walipokusanyika askari
hao na baadaye kuelekea Hospitali ya Muhimbili. Hata hivyo, wanahabari
walishindwa kuzungumza na mwenyekiti huyo kwa sababu za kiusalama.
VITA VYA URAIS CCM NJE NJE ... VIJANA KWA WAZEE WAPIGANA VIJEMBE
Na Mussa Juma, Mwananchi
Arusha. Wakati
joto la urais likizidi kupanda ndani ya CCM kutokana na hofu ya baadhi
ya majina mazito ya wagombea wa nafasi hiyo kukatwa kwa mizengwe, vita
vya wagombea sasa ni dhahiri baada ya mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kusema
hakuna mtu atakayekatwa bila ya sababu za msingi.
Mjumbe huyo, Sadifa Juma Hamisi, ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Vijana
wa CCM (UVCCM), pia alisema umoja huo haujafikia uamuzi wala kumtuma
mtu kumdhibiti mwanachama anayetajwa kuwania urais.
Katika siku za karibuni kumekuwapo mjadala mkubwa ndani ya CCM juu ya
mtu atakayepitishwa kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho, na ilizidi
baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa mwanachama ambaye atateuliwa
na CCM kugombea urais hayumo miongoni mwa waliojitokeza na kuwataka
wanachama kuwashawishi watu wenye sifa wajitokeze.
Siku chache baadaye, Dk Raphael Chegeni aliliambia gazeti la Mwananchi
kuwa ametumwa na wanachama wa CCM wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda
kumshawishi Lowassa kujitokeza kuwania urais kuitikia wito wa Rais
Kikwete wa kuwataka wanachama kuwashawishi watu wenye sifa kujitokeza.
Hadi sasa, wanachama waliojitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea
urais ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda, January Makamba (Naibu Waziri wa
Sayansi na Teknolojia), Hamisi Kigwangala, na Lazaro Nyalandu ambaye ni
waziri wa Maliasili na Utalii.
Lakini pia wako wanaotajwa kuwania urais lakini hawajatangaza ambao ni
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sita, William Ngeleja,
Emmanuel Nchimbi, Mwigulu Nchemba, Stephen Wasira, Bernard Membe na
Edward Lowassa ambaye ameibua mjadala kati ya kambi yake na
zinazompinga.
Mapema wiki iliyopita, katibu wa uhamasishaji na chipukizi wa UVCCM,
Paul Makonda alikaririwa akisema kuwa vitendo vyake vya kumshambulia
Lowassa vinatokana na kutumwa na umoja huo kumdhibiti, jambo ambalo
limezidisha mjadala kuhusu mteule wa chama hicho.
Kutokana na hofu hiyo, viongozi wa UVCCM na CCM mkoani Arusha wametuma
ujumbe wa maneno kwa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa za chama
hicho wakitaka wanachama wasifanyiwe kile wanachokiita kuchafuana na
vitisho vya baadhi ya wagombea kukatwa kimizengwe.
Ujumbe huo ulitumwa juzi na mwenyekiti wa CCM wa mkoa, Onesmo ole
Nangole na mwenyekiti wa UVCCM, Robinson Meitinyiku ambao walitaka
Sadifa Juma Hamis kueleza msimamo wa mkoa kwa vyombo hivyo viwili vya
maamuzi, na mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM aliwahakikishia kuwa hakuna
mgombea atakayekatwa kwa “sababu za kijinga”.
Akijibu ujumbe wa viongozi hao, Sadifa aliyekuwa jijini hapa kumsimika
kamanda wa vijana wa wilaya ya Arumeru, Mathias Manga, aliwaondolea hofu
katika hafla hiyo akisema hakuna mgombea wa urais wa CCM ambaye
atakatwa bila sababu za msingi, lakini akawataka vijana kusubiri zamu
yao hadi 2025.
Kauli ya Sadifa
“Niwaombeni mwenyekiti wa mkoa na mwenyekiti wa UVCCM, msiogope. Hakuna
mtu atakayekatwa kijinga ndani ya Kamati Kuu au Halmashauri Kuu. Kikubwa
tufuate maadili. Mimi mchapakazi ndiye nitamtetea,” alisema bila kutaja
mgombea anayekusudiwa.Alisema
ni lazima kiongozi bora awe na mikakati na dira na upeo wa kuwa na
mikakati bora ya kutekeleza ahadi zake kwani hatuwezi kuwa na kiongozi
ambaye hana dira wala mikakati.
“Tunataka kiongozi mwenye kujiamini, awe ana vision (dira) na mission
(mikakati), msikivu... hatuwezi kuchagua rais ambaye hana sifa hizi,”
alisema.
Akizungumzia maombi ya Nangole kuhusu tabia ya kuwachafua baadhi ya
wagombea na kuwatisha, Sadifa alisema hakuna kiongozi aliyetumwa na CCM
na UVCCM kutukana mtu wala kumtisha.
“Mzee wangu, watu wengi wanajua wanamtaka nani, ukiona mtu anapanda
kwenye majukwaa anamchafua mwenzake, ujue huyo ana mapungufu ya malezi,
hakuna haja ya kumjibu kwani utaonekana na pia wewe una mapungufu,”
alisema.
Akionekana kujibu kauli ya Makonda, Sadifa alisema UVCCM haijatuma mtu
amtukane mwingine. Alisema akiwa mjumbe wa Kamati Kuu, hawajawahi
kumtuma kiongozi yoyote kumtukana mwanachama mwingine wa CCM.
Alipoulizwa kuhusu hofu hiyo, kwa kifupi katibu wa itikadi na uenezi wa
CCM, Nape Nnauye alisema: “Mimi siwezi kuwa msemaji wa Umoja wa Vijana,
nikisema niwajibu nitakuwa nimepotoka.”
Mapema wiki iliyopita, Makonda alikaririwa akisema kuwa amekuwa
akimshambulia Lowassa, ambaye anatajwa kuwania urais kupitia CCM, kwa
sababu ametumwa na umoja huo.
Makonda amekuwa akikaririwa mara kwa mara akisema kuwa Lowassa hafai
kuwa mteule wa CCM wa kuwania urais na mikanda ya kauli zake imesambaa
kwenye mitandao ya kijamii, jambo lililofanya uteuzi wake kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni uhojiwe na watu wengi na hivyo kujikuta akilazimika
kusema ametumwa na umoja wake kumdhibiti waziri mkuu huyo wa zamani.
Katika mazungumzo yake juzi, Sadifa hakutaka kutaja jina la mgombea
atakayemtetea wala mtu anayemshambulia, badala yake alisema muda
ukifika, kila kitu kitajulikana kwa kuwa watu wanamjua mgombea
wanayemtaka.
“Mwenyekiti, dawa ya mjinga ni kukaa kimya, watu wanamjua mtu ambaye
wanamtaka. Rais Jakaya Kikwete ni mtu ambaye hatabiriki, hana
ushemeji... nyie subirini tu wakati ukifika,” alisema.
Vijana na urais
Akizungumzia vijana ambao wanautaka urais, Sadifa aliwataka kusubiri zamu yao hadi 2025 ili wazee waliopo wamalize muda wao.
Alisema utakapofika mwaka 2025 vijana watakuwa katika nafasi nzuri sana
ya kushika uongozi na hawatakubali kuona viongozi wazee wakitaka kupewa
nafasi.
“Wazee tutawaomba radhi mwaka wenu ni 2015 hadi 25, mkimaliza hapo, miaka yenu imekwisha, msije tena,” alisema.
Kauli ya Nangole
Awali, Nangole, ambaye aliwahi kusema kuwa Lowassa ni kiongozi msikivu
na makini na ambaye ni tegemeo la Watanzania katika kuwaunganisha kuwa
kitu kimoja, aliomba Kamati Kuu ipelekewe ujumbe kuwa CCM mkoani Arusha
hairidhishwi na matendo ya baadhi ya viongozi kuwatukana na kuwatisha
wengine.
Nangole alirejea kauli aliyowahi kuitoa kuwa CCM ni ya wanachama wote na
ndani yake hakuna sisimizi au tembo wa kumtisha mwingine ili mradi
anafuata taratibu za chama hicho.
Alisema imeibuka tabia ya baadhi ya viongozi wa CCM, kuwatisha wengine
na kuwatukana kana kwamba wao ndio wana hatimiliki ya CCM.
Naye mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha, Robinson Meitinyiku alisema kuna
kiongozi mmoja ametoa kauli kuwa mgombea mmoja hata kama akisafishwa na
madodoki hawezi kuwa msafi.
Badala yake alisema kiongozi aliyetoa maneno hayo ndiye hawezi
kusafishika hata kwa gunzi kwani kuna taarifa aliwahi kusaliti na
kujiunga na chama kingine.
Sunday, 22 February 2015
CHADEMA YATIKISA SUMBAWANGA
Kati ya mitaa 44 ya sumbawanga mjini chadema mpaka sasa imetangazwa ushindi kwenye mitaa 34 huu ulikuwa ni marudio ya uchaguzi... kwa mahesabu zaidi ya mji mdogo huwo wa sumbawanga nawaachia ccm wapige mahesabu.
Kinachoendelea sumbawanga sasa....
Uchaguzi Mitaa 44 Ya Kata 3 Sumbawanga Mjini Leo Tar 22.02 CCM INA MITAA 4 PAMOJA NA 1 WALOWEKA PINGAMIZI, CHADEMA INA MITAA 39...
GABRIEL MWANG'ONDA NA UCHAMBUZI WA KIUCHUMI SEKTA YA MAFUTA TANZANIA
In Tanzania edible oil is the second most expensive commodity that we import after refined petroleum products.
Our balance of payments is not in a good shape because of these two
products,Leave alone petroleum products which we might,(just incase we
find any) do away with.
Sasa kwa hili la palm oil (mawese) sioni ni wapi tunakwama mpaka tunashindwa kujitosheleza. Mawese Ya Kigoma kwa akina Zitto Kabwe na kwetu kule Kyela yakilimwa kwa ustadi na utaalamu tutaondokana na tatizo
kubwa la ajira,tutabakiza fedha zetu nchini,ulali wa biashara za nje
utaimarika,serikali itapata fedha nyingi tu kwa njia Ya kodi.
Uthibiti uliopo kwenye sekta Ya sukari basi uwepo hata huku,uwezo tunao
lakini sera nazo inafaa ziwe na upendeleo kwetu ili tulime kisasa na
kuhakikishiwa soko la ndani na nje.
Mahitaji ni MT-350k kwa mwaka hii ni biashara kubwa kabisa nchini na ku export kabisa,sasa tumebaki kuinunua toka mbali sana..hii product inaweza Kabisa ikawa ni chanzo Cha forex-inawezekana timiza wajibu wako.
Ni ndoto kama ningekua Magogoni
GM

Saturday, 21 February 2015
STOP ALBINO KILLINGS,,,,CAMPAIGN
There
is more to life than uniformity. .. The Preciousness of Albino is in
protecting their lives and rising above the Mediocrity that comes with
superstition and the Madness it encompasses.
Other albino species are the beauty of nature, Protect Albinos Tz. Let's make noise about it and #StopThisMadness
Other albino species are the beauty of nature, Protect Albinos Tz. Let's make noise about it and #StopThisMadness
NYINGE NAZARENO NJIA PANDA KUGOMBEA DODOMA MJINI AU KALENGA
Nazareno Nyinge: Anasema
"Wakati
nafanya tathmini ndogo ya kusimama kupigania jimbo la dodoma mjini
naangalia kwa jicho la mwewe jimboni kwangu nilikozaliwa KALENGA ambapo
fadhila zimetumika kurithisha madaraka pasipo kujali huruma ya wananchi
wanaotaka mabadiliko napata shida sana na cjui nisimame wapi kote hali
ngumu
1. wanawake wanapata shida mahospitalini
2. miundombinu kwao ni hadithi husikia kwenye taarifa ya habari tena kupitia radio ya m/kiti wa mtaa
3. huduma za jamii nashukuru kwa kuwa mungu aliweka vyanzo vya maji hivyo wanakunywa maji meupe yasiyo salama
4. kufanya mabadiliko wanatishiwa kutatokea vita
5. kofia na khanga imekuwa ndiyo hongo kwao
6. napata uchungu kuona wanafunzi wanakaa chini mpaka miaka zaidi ya 50 baada ya kuwa huru
7.kenya wanafanya jitihada angalau kila mwanafunzi awe na computer yake
wakati tanzania tunasema angalau kila mwanafunzi awe na dawati
nathubutu bila kuwa na maslahi yeyote kwamba sintoacha hata chembe ya
sekunde ya muda kupotea nitapigana mpaka mabadiliko ya kweli na ukombozi
wa kweli unapatikana
vijana tubadilishe fikra zetu kwa kutokujikitaa sana kushabikia vyama tuweke watu wanaoweza kuleta mapinduzi ya kweli
viwanda kurudisha
rasili mali kupewa nafasi kutumika na wananchi tabaka zote kwa usawa
wananchi kujivunia kile kilichochao daima....young generation forever...
President Kagame meets with Federal Foreign Minister of Germany
President Kagame meets with Federal Foreign Minister of Germany,Frank-Walter Steimmeier during his working visit to Rwanda.
For more pictures: https://www.flickr.com/phot…/paulkagame/…/72157650884180726/
For more pictures: https://www.flickr.com/phot…/paulkagame/…/72157650884180726/
UN:WANAOENDESHA UHALIFU SYRIA KUTAJWA,,,, SOMA HAPO CHINI
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa
wanapanga kuchapisha majina ya takriban watu 200 wanaotuhumiwa kuendesha
uhalifu wa kivita nchini Syria.
Tume huru ya uchunguzi ya umoja wa mataifa inasema kuwa kumekuwa na ongezeko la uhalifu nchini humno.
Majina
yanayojumuisha wakuu wa kijeshi , wasimamizi wa magereza na makamanda
wa makundi yasiyokuwa ya serikali yaliyo na silaha tayari yamewasilishwa
kwa tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataifa.
Serikali ya Syria hatahivyo imekataa kutoa ushirikiano kwa tume hiyo.
Umoja
wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 220,000 wameuawa nchini Syria na
mamilioni ya wengine wamehama makwao wakati wa mazozo wa miaka minne .
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimia miaka 91 leo
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimia miaka 91 leo.
Yeye sasa ni kiongozi mzee kabisa duniani, na amekuwa madarakani kwa miaka 35.
Sherehe ya siku yake ya kuzaliwa itafanywa juma lijalo.
Anatarajiwa
kufanya sherehe kubwa katika uwanja wa golf huko Victoria Falls,
inakisiwa sherehe yenyewe itagharimu dola milioni moja.
Maelfu ya watu watahudhuria karamu hiyo, ambapo kutachinjwa ndovu, nyati, paa na simba mmoja.
Shirika la habari la taifa linasema wananchi watalipia dhifa hiyo
Zimbabwe ni moja kati ya nchi maskini duniani.
Friday, 20 February 2015
KAULI NZITO YA KADA WA CHADEMA JUU YA MAUUWAJI YA ALBINO
Remija Wa Yesu
Nimesikitishwa sana na mauaji ya mtoto Yohana Bahati!! Mauaji ya kinyama kabisa, ninalaani mauaji haya.
Ninachojiuliza kama serikali inatumia pesa nyingi kujenga mahospitali
na kuajiri madaktari, na inasema haiamini katika uchawi, sasa hawa
waganga wa kienyeji na wachawi wanatoka wapi? Kwanini wanasajiriwa?
Kwanini wapo kwa tiba zipi? Mbona haya mahospitali hawajawahi kutoa
rufaa wagonjwa waende kutibiwa kwa waganga wa kienyeji?
Utasikia watasema tuwalinde albino, tuwapeleke kwenye mashule fulani, tusiwaache peke yao, kwanini hawa wachawi wasizuiliwe kufanya kazi zao? Watu wajiishie kwa rahaaa.
Utasikia watasema tuwalinde albino, tuwapeleke kwenye mashule fulani, tusiwaache peke yao, kwanini hawa wachawi wasizuiliwe kufanya kazi zao? Watu wajiishie kwa rahaaa.
Ninachoshangaa na kujiuliza zaidi watanzania wote isipokuwa wachache
sana: niliwahi kuambiwa, nilipokuwa mdogo Kingunge tu ndio haamini
katika dini hizi, ila sijathibitisha mpaka leo, na katika kukua kwangu
mpaka leo sijakutana na MTU mpagani, ila wote sisi ni wakristo na
waislamu tena waumini wazuri wa kuhudhuria kwenye nyumba za ibada,
inakuwaje hawa waganga wapo na wanapata wateja? Ni Mungu yupi
tunayemwabudu? Au ndio michanganyo, mungu baali kidogo na Mungu muumba
Mbingu na Nchi kidogo.
Ningekuwa rais ningefutulia mbali waganga wote.
RIP Yohana Bahati kilio cha damu yako kitafika Mbinguni!!!!!
Ningekuwa rais ningefutulia mbali waganga wote.
RIP Yohana Bahati kilio cha damu yako kitafika Mbinguni!!!!!
Rais Jakaya Kikwete akabidhiwa rungu la Afrika Mashariki,,,,, Jijini Nairobi
Marais Wa Afrika Mashariki Kutoka Kushoto Ni Mh.Pierre Ngurunzinza Wa Burundi,Mh.Jakaya Mrisho Kikwete Wa Tanzania, Mh.Uhuru Muigai Kenyatta Wa Kenya, Mh.Yoheri Museven Wa Uganda na Paul Kagame Wa Rwanda Leo Hii Jijini Nairobi
Rais Paul Kagame Na Hasimu Wake Rais Kikwete Na Mwenyeji Wa Rais Uhuru Wa Kenyatta Kabla ya kikao
Rais Wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta
Akimkabidhi Rais Wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete Uwenyekiti wa
Jumuia ya Afrika mashariki Leo Hii Jijini Nairobi.
Mh.Uhuru Kenyatta akimpokea Mh Kikwete Jijini Nairobi
Rais Wa Kenya Uhuru Akimpokea Rais Wa Uganda Mh. Mseven
Baadhi ya Marais Wa Jumuiaya ya Afrika Mashariki Wakiwa pamoja na makamu wa Rais wa Kenya Mh.Ruto Kabla ya Mkutano
Rais Uhuru Na Pierre Ngurunzinza Wakisalimiana
Rais Uhuru Kenyatta Wakisalimiana na Paul Kagame
Picha kwa hisani ya Nombees toka Nairobi