Wednesday 18 February 2015

Askari wa usalama barabarani wakusanya mapato badala ya kulinda usalama

 


OPERESHENI ya kukamata madereva wa magari wanaofanya makosa ya barabarani, inayoendana na utozaji wa tozo za faini, imewaondoa Askari wa Usalama Barabarani, kwenye jukumu lao la msingi la kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara, na kuwapeleka kwenye ukusanyaji wa mapato unaotiliwa shaka kiasi cha kuibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa barabara nchini.
Uchunguzi uliofanywa na World over challenge kwa siku kadhaa sasa umebaini kuwepo kwa mbinu za askari hao wa usalama barabarani kujificha vichakani ili tu kukamata magari yanayokiuka taratibu za matumizi ya barabara kwa lengo la kujipatia fedha, hali inayotia shaka kama fedha zote zinazokusanywa na askari hao zinaingia kwenye mfumo wa mapato ya Serikali au nyingine zinaishia mifukoni mwao.
Malalamiko ya madreva wa magari
Baadhi ya madereva katika maeneo mbalimbali nchini wamelalamikia kitendo cha askari hao kuwakamata na kuwaamrisha kulipa faini za papo kwa hapo badala ya kuwaelimisha wakosaji juu ya baadhi ya mambo wanayokosea wakiwa barabarani. Kwa mujibu wa madereva hao, si kila kosa linalofnyika barabarani linatakiwa litozwe tozo, bali yapo baadhi ya makosa ambayo dereva anapaswa kukamatwa na kuelimishwa tu bila kuadhibiwa.
Wanayataja baadhi ya makosa ambayo yanahitaji kukumbushwa tu kwa madereva, kama sheria ya usalama barabarani ya mwaka 2011 inavyosema kuwa ni pamoja na dereva na abiria wake kusahau kufunga mkanda na magari ya kubeba abiria kutoandikwa jina ubavuni.

No comments:

Post a Comment