OPERESHENI ya kukamata madereva wa magari wanaofanya makosa ya
barabarani, inayoendana na utozaji wa tozo za faini, imewaondoa Askari
wa Usalama Barabarani, kwenye jukumu lao la msingi la kuhakikisha
usalama wa watumiaji wa barabara, na kuwapeleka kwenye ukusanyaji wa
mapato unaotiliwa shaka kiasi cha kuibua maswali mengi miongoni mwa
wadau wa barabara nchini.
Uchunguzi uliofanywa na World over challenge kwa siku kadhaa sasa umebaini kuwepo kwa mbinu za askari hao wa usalama
barabarani kujificha vichakani ili tu kukamata magari yanayokiuka
taratibu za matumizi ya barabara kwa lengo la kujipatia fedha, hali
inayotia shaka kama fedha zote zinazokusanywa na askari hao zinaingia
kwenye mfumo wa mapato ya Serikali au nyingine zinaishia mifukoni mwao.
Malalamiko ya madreva wa magari
Baadhi ya madereva katika maeneo mbalimbali nchini wamelalamikia
kitendo cha askari hao kuwakamata na kuwaamrisha kulipa faini za papo
kwa hapo badala ya kuwaelimisha wakosaji juu ya baadhi ya mambo
wanayokosea wakiwa barabarani. Kwa mujibu wa madereva hao, si kila kosa
linalofnyika barabarani linatakiwa litozwe tozo, bali yapo baadhi ya
makosa ambayo dereva anapaswa kukamatwa na kuelimishwa tu bila
kuadhibiwa.
Wanayataja baadhi ya makosa ambayo yanahitaji kukumbushwa tu kwa
madereva, kama sheria ya usalama barabarani ya mwaka 2011 inavyosema
kuwa ni pamoja na dereva na abiria wake kusahau kufunga mkanda na magari
ya kubeba abiria kutoandikwa jina ubavuni.
No comments:
Post a Comment